Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kijana wa umri wa makamo alifikishwa katika mahakama ya Mombasa na kufunguliwa mashtaka ya kutekeleza wizi wa mabavu.

Upande wa mashtaka uliiambia mahakama siku ya Jumanne kuwa Ali Henry anadaiwa kujihami kwa panga na kumvamia na kumuibia Justus Mulwa.

Mshukiwa anadaiwa kuiba simu yenye thamani ya shilingi elfu 90 ikiwa mali ya Mulwa.

Henry alikanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu Samuel Rotich.

Hakimu Rotich alisema kuwa kulingana na katiba, iwapo mshukiwa atapatikana na makosa ya wizi wa mabavu basi atahukumiwa kunywongwa.

Kesi yake itasikilizwa tena Januari 12, 2016.