Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Msichana mmoja wa umri wa miaka 14 kutoka kijiji cha Rinyenga wilayani Borabu kaunti ya Nyamira amefariki baada ya kuanguka ndani ya kisima chenye futi 70.

Akitibithisha kisa hicho siku ya Jumapili, mkuu wa polisi wilayani Borabu Athony Onyango alisema msichana huyo alikuwa akichota maji kwenye kisima hicho na kwa bahati mbaya akateleza na kuanguka ndani.

Juhudi za kumuokoa hazikufaulu.

“Msichana huyu alikuwa anachota maji na aliteleza na kuanguka ndani na kufariki papo hapo,” alisema Athony Onyango, mkuu wa polisi Borabu

Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi chumba cha kuhifadhi maiti cha Nyansiongo .