Mtoto wa mshukiwa wa mauwaji ya Mpeketoni Ali Mahadi Swaleh ameiambia mahakama kuwa babake hakuwa Mpeketoni wakati wa mauwaji hayo mwaka 2014.
Ali Mahadi Swaleh aliiambia mahakama kuu siku ya Alhamisi kuwa walikuwa pamoja na babake, Mahadi Swale, wakitazama mpira wa kombe la dumia mwaka 2014 katika nyumba yao huko Malindi.
Aidha, amekanusha madai kuwa babake alihusika na mauwaji hayo ya Mpeketoni.
Siku ya Jumatano, dereva wa tuktuk Samuel Mwangi alithibishia mahakama kuu kuwa mfanyibiashara Mahadi Swaleh hakuhusika katika mauwaji hao.
Akitoa ushahidi wake katika mahakama kuu ya Mombasa, Swaleh ameiambia mahakama kuwa wakati wa shambulizi la Mpeketoni alikuwa pamoja na mshukiwa nyumbani mwake Malindi, thibitisho tosha kuwa hakuwa Lamu na hakutekeleza mauwaji hayo.
Siku ya Jumatatu wiki iliyopita, Swaleh alikanusha kuhusika na mauwaji hayo na kuitaja hatua hiyo kama njama ya kumchafulia jina ikizingatiwa yeye ni mwanabiashara maarufu kaunti ya Lamu.
Naye Diana Salim aliambia mahakama kuwa akiwa na wenzake walivamiwa na wanamgambo hao katika eneo la Mambosasa na kulazimishwa kusoma suratul Fathia.
Mwanadada huyo aliongeza kuwa wenzake wawili walipigwa risasi baada ya kutambulika kuwa si waislamu.
Alisisitiza kuwa gari zao mbili aina ya matatu zilichukuliwa na wanamgambo hao baada ya kuwavamia.
Mahadi Swaleh na Diana Salim wanakabiliwa na kesi ya ugaidi na mauwaji ya watu 60 kwenye shambulizi liliotokea Mpeketoni mwaka 2014.