Share news tips with us here at Hivisasa

Kinara wa chama cha National Amani Congress (NAC) Musalia Mudavadi, amewarai viongozi wa dini ya Kiislam eneo la pwani kumuunga mkono katika azma yake ya kuwa rais wa Kenya.

Mudavadi amewataka viongozi waKiislam kuhakikisha kuwa wafuasi wao wanajitokeza kwa wingi kumpigia kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

Akizungumza na wanahabari siku ya Jumamosi baada ya kufungua afisi ya chama hicho mjini Mombasa, Mudavadi amesema kwamba serikali ya Jubilee imeshindwa kuwafanyia Wakenya maendeleo na badala yake kuendeleza ufisadi nchini.

Amewataka wakazi wa eneo la Pwani kujiepusha na viongozi wasio na azma ya kueleta maendeleo nchini na kuwachagua viongozi waadilifu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

“Ninawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi na kunichagua kama rais wa taifa la Kenya katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2017 ili tubadilishe uongozi wa taifa hili kwani yale tunayoyashughudia yanazidi kudidimiza uchumi wa nchini,” alisema Mudavadi.

Mudavadi alikuwa ameandamana na naibu kiongozi wa chama hicho Kasim Tandaza pamoja na katibu mkuu Justus Kizito.