Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Kasisi wa kanisa la katoliki mjini Kisii Vincent Simba amewashauri wazazi kutowalazimisha watoto wao ambao walifanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana kurudia masomo yao kwa misingi ya kuwa hawakufanya vyema katika mtihani huo.

Kulingana na kasisi huyo aliyezungumza na mwandishi huyu aliwahimiza wazazi kuwapeleka watoto hao katika vyuo vya kiufundi ili wajiendeleze kielimu kwani huenda watafanya vizuri katika vyuo hivyo na kujiimarisha kimaisha.

“Naomba wazazi wenye watoto ambao hawakuhitimu kujiunga na vyuo vikuu na ata vyuo vya kati wawapeleke katika vyuo vya anuwai kufanya taaluma za kiufundi na kujiendeleza,” alisema Simba.

“Mzazi anapomlazimisha mtoto kurudia masomo huwa ni jambo ambalo halizalishi matunda bora maana kuna uwezekano kiwango cha mwafunzi huyo kilifikia penye alifikisha alama yake,” aliongeza Simba.

Aidha, Kasisi Simba aliomba wazazi kuhakikisha watoto wao wamepata la kufanya na kutokaa nyumbani bila chochote ili kupunguza umaskini katika jamii mbalimbali.