Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwakilishi wa wadi ya Marani, kaunti ya Kisii Dennis Ombachi ameomba serikali ya kaunti ya Kisii kueleza kwa nini kiwanda cha kusaga majani chai katika eneo la  Sombogo hakijaanzishwa kujengwa hadi sasa.

Kiwanda hicho kilipendekezwa kujengwa miaka mitano iliyopita, lakini hakuna ishara yoyote imeonekana kuwa kitajengwa, jambo ambalo lilimpelekea mwakilishi huyo kuomba serikali kueleza kwa nini ujenzi huo haujaanza.

Akizungumza na mwandishi huyu wa habari mnamo siku ya Jumatatu, Ombachi alisema serikali ya kaunti ya Kisii ilitenga millioni 30 ambazo zingegharamia ujenzi wa kiwanda hicho cha majani chai, lakini kufikia sasa hakuna lolote limeonekana kufanywa.

Sasa mwakilishi huyo ameitaka serikali ya Kisii kueleza kwa nini ujenzi huo haujaanzishwa.

 Aidha, aliomba serikali kujaribu kila iwezalo kuwahurumia wakulima wa mumea huo na kujenga kiwanda hicho ili kuwapa wakulima wa mumea huo afueni.

“Naomba serikali ya kaunti kushirikaiana na chama kinachowasimamia wakulima wa majani chai cha KTDA kujenga kiwanda cha eneo la Sombogo, maana kimechukua mda mrefu zaidi bila kujengwa, na shamba liko kubwa ambalo wakulima walinunua,” alisema Ombachi.

“Wakulima wetu wamekuwa wakisumbuka sana kwa kukaa kwa vituo vya kununua majani chai kwa kutochukuliwa kwa majani  chai yao, na kulifikisha jambo hili mwisho sharti serikali ya kaunti ya Kisii na chama cha KTDA kushirikiana kujenga kiwanda ilivyopendekezwa hapo mbeleni,” aliongeza.