Share news tips with us here at Hivisasa

Mwakilishi wa Wadi ya Elburgon Florence Wambui ametoa wito kwa vijana katika eneo hilo kuungana na kuepuka kutumiwa na wanasiasa.

Akizungumza siku ya Jumamosi katika soko la Elburgon, Wambui alisema kuwa vijana wanaweza jiimarisha tu iwapo wataungana na kuwa kitu kimoja.

"Mimi nataka niwaeleze vijana kwamba nyinyi ni watu wa maana sana lakini mnafaa kujiimarisha kwa kuungana," alisema Wambui.

Wakati huo huo, mwakilishi huyo aliwasuta wale ambao wanaendeleza siasa potovu kwamba chuma chao ki motoni.

Alisema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakimkosoa Gavana Kinuthia Mbugua pasina misingi yoyote.

Alitoa wito kuwa viongozi wa kisiasa Nakuru kukumbatia siasa komavu za kuunganisha makabila yote ya Nakuru.