Mwakilishi wa wadi ya Biashara kaunti ya Nakuru Stephen Kuria , anakabiliwa na mashtaka ya uchochezi wa umma kwa minaajili ya kuharibu vibanda vilivyokuwa vinajengwa mjini Nakuru.
Mwakilishi huyo anadaiwa kuchochea umma kwa lengo la kuzua ghasia mnamo Juni 20, 2015 uliopita katika jumba ka KANU mjini Nakuru.
Mwakilishi huyo akiwa mbele ya Hakimu mkuu Doreen Mulekyo Jumanne alikanusha mashtaka dhidi yake.
Kadhalika mwakilishi huyo anadaiwa kutamka matamshi yaliyodhihirisha dharau kwa mahakama baada ya mahakama hiyo ya Nakuru kutoa amri iliyozuia vibanda hivyo visibomolewe , huku akisema amri hiyo ilikuwa ni karatasi tu, kama makaratasi mengine.
Kesi hiyo itaskizwa Februari 26.