Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Polisi Mjini Malindi wanamzuia mwamachama wa ODM Kassim Mwapojo, ambaye pia ni mwakilishi wa Wadi ya Mereni katika eneo bunge la Lungalunga, kwa madai kuwa alikuwa anapanga njama ya kuiba kura katika uchaguzi mdogo wa Malindi.

Polisi walimtia mbaroni mwakilishi huyo usiku wa kuamkia siku ya Ijumaa, baada ya kupokea taarifa kuwa anadaiwa kupanga njama na maafisa wa Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), ya jinsi watakavyoiba kura hizo.

Inaripotiwa kuwa polisi walifanya msako katika chumba chake katika hoteli moja mjini Malindi, pamoja na katika gari lake lakini hakuna chochote kilichopatikana.

Kwa sasa, polisi wanazuia simu yake huku wakifanya uchunguzi zaidi.

Viongozi wakuu wa chama cha ODM kutoka Kaunti za Kilifi na Mombasa wakiongozwa na kinara wa chama hicho Raila Odinga, kwa sasa wamepiga Kambi katika Kituo cha polisi cha Malindi.