Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hatua ya waziri wa elimu nchini Fred Matiang'i kutishia kuvunja bodi simamizi katika shule za umma kwa madai ya kuingisha siasa kwenye uongozi wa shule hizo imeungwa mkono na mwalimu mkuu wa shule ya upili mseto ya Gesiaga Sarah Mang'aa.

Akihutubia wanahabari pindi baada ya kupokea rasmi matokeo ya mtihani ya kidato cha nne mwaka jana siku ya Ijumaa, Mang'aa alisema yafaa bodi simamizi za shule zinazoingisha siasa za ukabila shuleni zivunjiliwe mbali kwa maana hali hiyo huchangia matokeo duni kwenye mitihani ya kitaifa. 

"Bodi ambazo huingisha siasa kwenye usimamizi wa shule za umma zastahili kuvunjiliwa mbali kwa maana kwa hakika siasa za aina hiyo huathiri pakubwa masomo kwenye shule za umma," alisema Mang'aa. 

Mang'aa aidha alifurahia matokeo ya shule hiyo kwa kuwashkuru washikadao walioshirikiana kuhakikisha wamepata maki ya wastani 7.8. 

"Kwa kweli tumefurahi sana kwa jinsi ambavyo wanafunzi wetu walivyofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana kwa maana tulifanikiwa kupata alama ya wastani 7.8," aliongezea Mang'aa.