Mahakama ya Mombasa hatimaye imemhukumu mwalimu wa dini kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kupatikana na hatia ya kutoa mafunzo ya itikadi kali.
Mshatakiwa, Salim Mohamed Wabwile, alishtakiwa kwa madai ya kutoa mafunzo hayo ya itikadi kali katika msikiti mmoja kule Kaloleni.
Akitoa uamuzi huo siku ya Alhamisi, Hakimu wa Mombasa Diana Mochache alisema kuwa mahakama imethibitisha kuwa mshukiwa alikuwa na hatia.
Hapo awali mwalimu huyo alikanusha madai ya mwanafunzi mmoja aliyetoa ushahidi mahakamani na kuambia mahakama kuwa mwalimu huyo alikuwa akiandika maandishi ya itikadi kali kwenye shati zao.
Wabwile aliyeshtakiwa mahakamani humo mnamo Juni mwaka wa 2015, amepewa siku 14 kukata rufaa.