Mwanabiashara mwengine amefikishwa mahakamani Mombasa na kufunguliwa shtaka la kuingiza sukari kinyume cha sheria nchini.
Siku ya Jumatano, Abdikadri Osman Mohamed alidaiwa kuingiza makasha matano ya sukari yenye thamani ya shilingi milioni tisa kutoka Brazil kupitia bandari ya Mombasa mnamo Septemba 17,2015.
Mshatakiwa Abdikadri alikanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu Diana Mochache.
Mahakama ilimwachilia kwa dhamana ya shilingi 500,00 ama dhamana ya pesa taslimu shilingi 300,000.
Kesi hiyo itatajwa Machi 3, 2016 ili kuchanganywa na kesi sawia na hiyo.
Visa vya wafanyabiashara kuingiza bidhaa nchini kinyume na sheria vimeongezeka kwa kiwango kikubwa, huku bidhaa nyingi sawaia na hizo zikiharibiwa na serikali.