Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwanamke mmoja kutoka kaunti ya Vihiga anapokea matibabu katika hospitali moja mjini Nakuru baada ya kuchomwa kwa mafuta taa kufuatia mzozo wa mapenzi.

Dorcas Awinja alipelekwa hospitalini baada ya hali yake kuendelea kudhoofika alipoondoka hospitalini huko vihiga. 

Kwa mujibu wa madaktari, mwanamke huyo ana majeraha ya aslimia 63 kwenye mwili wake. 

Awinja alisema ugomvi ulianza wakati mumewe alipokataa kupokea simu aliyokuwa akipigiwa na mwanamke mwingine. 

"Alipigiwa simu na mwanamke mwingine lakini akakataa kupokea hapo ndio nilijua kuna shida," Awinja alisema.

 Aliongeza kuwa mumewe pia alitumiwa ujumbe kwenye simu ambao uliashiria kwamba alikuwa na uhusiano wa mapenzi na mwanamke mwingine jambo ambalo lilizua ugomvi baina yao. 

Mkuu wa polisi eneo la Emuhaya Benson Kilonzo alithibitisha hayo lakini akasema mshukiwa bado hajatiwa mbaroni.