Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamke wa miaka 45 aliyekamatwa akisafirisha misokoto ya bangi katika kivuko cha feri cha Likoni amefikishwa mahakani na kufunguliwa mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya.

Mahakama ilielezwa siku ya Jumatatu kuwa Monica Aoko alipatikana na misokoto 359 ya bangi katika kivuko cha feri mnamo Novemba 2, 2015 akiwa na lengo la kusafirisha bangi hiyo hadi nchini Tanzania.

Aoko alikanusha madai hayo na kutozwa dhamana ya shilingi milioni moja na mdhamini wa kiwango sawa na hicho.

Mshukiwa huyo alinaswa na polisi katika kivuko hicho baada ya mwananchi kuwaaarifu maafisa wa usalama kuhusu mshukiwa huyo.

Kesi yake itasikilizwa tena Desemba 23, 2015.