Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwanamke wa umri wa makomo amefikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la kuavya mimba.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Ijumaa kuwa mshtakiwa, Linet Kwamboka, anadaiwa kutekeleza kosa la kuavya mimba mnamo Januari 19, 2016, katika kambi ya jeshi ya wanamaji huko Mtongwe.

Mshtakiwa huyo alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Richard Odenyo na kupewa dhamana ya shilingi 100,000.

Kesi hiyo itasikilizwa tarehe April 4, 2016.