Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwanamme wa umri wa makamu ametiwa mbaroni katika eneo la Tala Kithimani baada ya kumshambulia nduguye na kumuumiza. 

Akithibitisha kisa hiki, Chifu was Kata ya Nguluni Johnbosco Ndambuki alisema kuwa mwanamume huyo alifika nyumbani na kumpata nduguye akilisha mifugo katika ardhi yake, na kumshambulia na kumpiga na kumuumiza baada ya kubishana kwa muda bila kufikia maelewano. 

Aidha, Ndambuki alielezea kuwa wawili hao wamekuwa wakizozania ardhi kwa muda mrefu, huku akilaani kitendo hicho kwa kusema kuwa watu was familia moja wanafaa kuongea na kuelewana na sio kuzua vurugu.

"Kuna njia nyingi za kutatua shida bila ya kuzua vurugu na kupigana hadi kuumizana," alisema Chifu huyo. 

Mwanamume huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Tala huku akisubiria kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu.