Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamme mmoja aliyepatikana na kosa la wizi wa mabavu na mahakama moja ya Nakuru amewasilisha rufaa mbele ya mahakama kuu ya Nakuru, kupinga uamuzi uliotolewa dhidi yake wa kifungo cha maisha.

Hii ni baada ya jamaa huyo kwa jina la Joseph Nyakundi kupatikana na kosa la kumwibia mwanamke mmoja kwa jina la Loise Wangechi shilingi 8,500 kwa kutumia mabavu mnamo tarehe 22 mwezi Agosti mwaka wa 2013 mjini Nakuru.

Jaji Maureen Odero na mwenzake Jaji J Mulwa waliokuwa wakisikiliza rufaa hiyo Jumanne hii ya tarehe 19 Januari hata hivyo waliahirisha kusikizwa kwake hadi mwezi Machi mwaka huu baada ya mwendesha mashtaka wa serikali kuomba mda wa kupitia rufaa huyo.

Kesi hii sasa itaskizwa tarehe kumi na mbili mwezi Machi mwaka huu.