Huku serikali ya kitaifa na ile ya kaunti ikikaza vita dhidi ya wafanyabishara wanaoleta bidhaa ghushi na kupakizwa katika bandari kuu ya Mombasa, mshukiwa mmoja anayetuhumiwa uingizaji bidhaa nchini yenye thamani ya shilingi milioni 14 katika eneo la Kilindini amefikishwa mahakamani mjini Mombasa siku ya Jumatano ambapo alikana madai hao ya kuleta bidhaa zilizopigwa marufuku.
Amos Kibagendi ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni 3 na mdhamini wa kiasi kama hicho na hakimu mkuu mwandamizi katika mahakama kuu ya Mombasa Richard Odenyo, ambapo kesi yake itasilikilizwa tarehe 5 mwezi wa nne.
Mshukiwa huyo ametuhumiwa kuwa mnamo tarehe 12 mwezi Oktoba mwaka 2015 katika eneo la Bandari kaunti ya Mombasa wakiwa na wengine hawakua mbele ya mahakama kinyume cha sheria waliingiza sukari ambapo ni kinyume cha utaratibu wa sheria za nchi.
Mshtakiwa huyo alipatikana na kosa jingine la kuingiza bidhaa zisizokubalika kisheria ambayo ni kinyume cha sheria ya thamani ya shilingi milioni 14 ambayo inadaiwa kuwa sukari iliyopakiwa kwenye mifuko ya plastiki.