Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume wa umri wa makamo alifikishwa mahakamani siku ya Jumatatu na kufunguliwa mashtaka ya kuiba kutoka benki.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama kuwa mnamo Oktoba 19,2015 mshtakiwa, Emmanuel Akendo, anadaiwa kuiba Sh487,000 kutoka kwa benki ya Barclays, tawi la Mombasa.

Hata hivyo, Akendo alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Diana Mochache na kutozwa dhamana ya Sh200,000.

Kesi hiyo itasikilizwa Aprili 7, 2015.