Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamme wa umri wa makamo amefikshwa katika mahakama kuu ya Mombasa kwa kosa la mauwaji.

Upande wa mashtaka uliambia mahakama kuwa mnamo Disemba 4, 2015, mshukiwa, Mohamed Bakari Bin anadaiwa kumuua Mahamoud Bakar katika eneo la Mwandoni.

Mohamed alikanusha mashtaka hayo ya mauaji siku ya Ijumaa mbele ya jaji Martin Muya, katika mahakama kuu ya Mombasa.

Kesi yake itasikilizwa Machi 4, 2016.