Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume wa umri wa makamo amefungwa miaka 12 gerezani kwa kosa la mauaji bila kukusudia.

Mshtakiwa, Sina Raha Baya, anadaiwa kumuua mwendazake Dama Katana mnamo Disemba 12, 2012, katika eneo la Maji Machafu huko Bamburi.

Akitoa hukumu hiyo siku ya Alhamisi, jaji katika mahakama kuu ya Mombasa, Martin Muya alisema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa ni wazi kuwa mshukiwa huyo alihusika katika mauaji hayo.

Mshtakiwa huyo alipewa siku 14 kukata rufaa kupinga kifungo hicho.