Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume wa umri wa makamo amehukumiwa miaka 4 gerezani kwa mastaka ya wizi .

Mshtakiwa Mohamed Hamisi Ali alipatikana na kosa la kuiba kitanda na vitu vingine vya nyumbani vya thamani ya shilingi 17,000 mnamo Agosti 8, 2015  huko Likoni.

Mshtakiwa alikiri madai hayo siku ya Jumanne mbele ya jaji Richard Odenyo wa mahakama ya kuu ya Mombasa.

Akitoa hukumu hiyo, jaji Odenyo amesema kuwa itakuwa funzo kwa wengine wanaojihusisha na wizi nchini.