Mwanamume mwenye umri wa miaka 45 amehukumiwa miaka mitatu gerezani kwa kosa la wizi.
Mshukiwa, Josephat Mogaka, anadaiwa kumuibia mwajiri wake Abdifatah Noor, mali ya duka yenye thamani ya shilingi 54,000 katika mtaa wa Ferry, eneo la Likoni, mnamo Mei 18, 2014.
Siku ya Jumanne, Mogaka alijitetea kwa kusema kuwa hakuwa na nia ya kuiba ila shetani ndiye aliyemshawishi kufanya kitendo hicho na kutaka mahakama kumsamehe.
Hakimu Richard Odenyo alimpa siku 14 za kukata rufaa.