Share news tips with us here at Hivisasa

Maafisa wa Polisi katika eneo la Likoni mjini Mombasa wanachunguza kisa kimoja ambapo mwili wa mwanamume mmoja ulipatikana katika chumba cha wageni kwenye mkahawa wa 'Capri bar and restaurant' siku ya Jumamosi.

Afisa Mkuu wa Polisi eneo la Likoni Willy Simba, alisema kuwa mwanamume huyo alikodi chumba hicho siku ya Ijumaa kwa mapumziko lakini baadaye alijitia kitanzi.

Simba alisema kuwa Wafanyikazi wanaosafisha vyumba katika mkahawa huo walikumbana na mwili wake ukining’inia juu ya dari na kuripoti mara moja kwa maafisa wa polisi.

“Tumepata kujua kuwa jamaa huyo ni mkaazi wa kaunti ya Meru na aliamua kujitia kitanzi kutokana na mgogoro wa ardhi lakini bado maafisa wetu waendeleza uchunguzi na ripoti kamili itatolewa," alieleza Simba.

"Lakini ningependa kuwaambia wananchi kutochukua hatua kama hiyo na iwapo kuna shida basi wawasiliane na maafisa husika," aliongeza Simba.