Share news tips with us here at Hivisasa

Mwili wa mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 38 umepatikana hivi leo Jumatatu umeninginia katika nyumba yake eneo la Kwa Mbui kata ya Kithimani. 

Akidhibitisha kisa hiki OCS wa Kithimani James Wairagu alisema kuwa kulingana na familia ya mwanamume huyo baada ya chakula cha chajio aliondoka kwenda kulala. 

Asubuhi ilipofika walimsubiri aamke ili aungane nao katika kiamsha kinywa ndipo walibisha mlango bila ya kujibiwa. 

Mlango wa nyumba hiyo ulipovunjwa ndipo mwili wake ulipatikana ukining'inia kwa kamba. 

Familia ya marehemu haijajua kilichomsukumia kujitia kitanzi kwani hakuacha barua nyuma. 

"Familia yake ilielezea kuwa haijui sababu inayowezakuwa ilimfanya kujitoa uhai kwani hakugombana na yeyote," alisema Wairagu. 

Mwili wa mwanamume huyo ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Matuu Median huku maafisa wa polisi wakianzisha uchunguzi.