Mwanamume wa umri wa makamo amekubali shtaka la kujirusha baharini katika kivuko cha feri cha Likoni.
Mshtakiwa, Martin Mwanzia, anadaiwa kujirusha baharini katika kivuko cha Likoni mnamo Februari 16, 2016.
Mshtakiwa huyo aliambia mahakama siku ya Alhamisi kuwa alifanya hivyo wakati alipokuwa mlevi na kuitaka mahakama kumsamehe.
Hakimu mkuu katika mahakama ya Mombasa Susan Shitub aliagiza ripoti kutoka kwa maafisa wa kubadilisha tabia kabla kutoa hukumu yake.
Shitub ameagiza mshukiwa huyo kuzuiliwa katika rumande ya Shimo la Tewa mpaka tarehe Machi 3, 2016, kusubiri ripoti hiyo.