Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanaume wa umri wa makamo anaendelea kupigania maisha yake katika Hospitali kuu Nyamira baada ya kula chakula kinachonakisiwa kuwa na sumu.

Kulingana na mkewe Jemimah Abuga ni kuwa jamaa huyo, Edwin Abuga, alifika nyumbani kwake siku ya Jumapili jioni na kukataa kula chakula, na kusema kuwa tayari alikuwa amekula kwenye mkahawa.

Bi Abuga alisema kuwa pindi tu mumewe alipoenda kulala, ndipo alipoanza kulalamikia kuumwa na tumbo pamoja na kichwa hali iliyo walazimu kuitisha gari na kumpeleka hospitalini.

"Tulishangaa sana baada yake kulalamikia maumivu makali ya tumbo ilhali hakuwa amekula nyumbani. Alikuja nyumbani na kwenda kulala tu baada yake kutueleza kuwa alikuwa amekula mkahawani na rafiki yake," alisema Abuga.

Mmoja wa maafisa wa masuala ya kliniki katika Hospitali kuu ya Nyamira Yvonne Onkundi, alisema kuwa muathiriwa alikuwa amekula chakula kilichokuwa na sumu.

Onkundi alisema wameanzisha vipimo kubaini aina ya sumu aliyokula mwathiriwa.

"Tayari tumebaini kuwa jamaa huyo alikuwa amekula chakula kilichokuwa na sumu ila sharti tufanye vipimo kubaini aina ya sumu aliyoila," alisema Onkundi.