Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwanamume mmoja alifikishwa katika mahakama ya Kisii na kushtakiwa kwa kosa la wizi wa mita za stima zinazotosha shillingi 25, 000.

Mwanamume huyo kwa jina Vincent Osoro alifikishwa mahakamani siku ya Jumatatu mbele ya jaji wa mahakama hiyo John Njoroge na kushtakiwa kwa kosa la wizi.

Ilisemekana kuwa mshtakiwa huyo alitekeleza wizi huo mnamo Novemba 25, 2015 kutoka kwa duka moja mjini Kisii.

Osoro alikana kosa hilo na baadaye akaachiliwa kwa dhamana ya shillingi 25,000.

Kesi hiyo ikizikizwa tena mnamo Januari 11, 2016.