Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume mmoja alifikishwa mbele ya Mahakama ya Mombasa kujibu shtaka la kumuibia mwajiri wake.

Upande wa mashtaka ulielezea mahakama siku ya Jumatatu kuwa kati ya tarehe 1 Aprili na Julai 25, 2015, mshtakiwa, Nicholas Kemboi, anadaiwa kuiba shilingi 95,045 mali ya Ben Choge.

Mshtakiwa alikana madai hayo mbele ya hakimu wa Mombasa Richard Odenyo na kupewa dhamana ya shilingi 10,000.

Kesi hiyo itasikizwa mnamo Machi 23, 2016.