Mwanamume wa umri wa makamo amefikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka ya kumbaka mwanamke mwenye akili taahira.
Upande wa mashtaka ulielezea Mahakama kuwa mtuhumiwa, Juma Ali Juma, anadaiwa kumbaka mjombake Mishi Ali, mwenye akili taahira huko Mtongwe.
Juma alikanusha mashtaka hayo siku ya Ijumaa, mbele ya hakimu mkuu wa mahakama ya Mombasa Susan Shitub.
Hakimu Shitub alimtoza dhamana ya shilingi 200,000.
Kesi hiyo itasikizwa mnamo Februari 16, 2016, mlalamishi atakapo pewa nafasi ya kutoa ushahidi wake.