Mwendeshaji pikipiki mmoja anaendelea kuuguza majeraha ya risasi baada ya kushambuliwa na wezi waliovamia duka la rejareja mtaani Kiwerera kaunti ya Mombasa.
Katika tukio hilo la Jumamosi, Jamaa huyo alijaribu kuwafwata wezi hao ambao walifanikiwa kuondoka na pesa taslimu 160 000.
Visa vya ukosefu wa usalama vimekithiri hivi majuzi ambapo watu wanaotumia usafiri wa pikipiki wamekuwa wakitekeleza uhalifu kwa kutumia bunduki.
Wakazi wa eneo hilo wameitaka kaunti ya Mombasa kuimarisha ulinzi wao na kuwakamata wahalifu wanaotumia bunduki kwenye eneo hilo.