Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hofu ilitanda katika kijiji cha Kabati mjini Naivasha Alhamisi, baada ya mzozo wa kinyumbani kati ya mwanamme mmoja na mkewe kugeuka na kuwa mauti, wakati mwanamme huyo alipatikana saa chache baada ya kumdunga kwa kisu mkewe.

Mwili wa mwanamme huyo ulipatikana kando ya barabara huku ukiwa na alama za kudungwa visu mara kadhaa mwilini katika kijiji hicho cha Kabati, wenyeji wakisema alijitoa uhai mwenyewe.

Walioshuhudia hayo wamesema kuwa marehemu alikuwa amemdunga visu kadhaa mwilini mke wake na alidhani amemuua ndiposa akaelekea kujitoa uhai.

Mkaazi mmoja Mary Njeri amesema kuwa wawili hao wamekuwa na mzozo wa kinyumbani na haijulikini kilichomsababishia kuchukua hatua hiyo.

Akidhibitisha hayo, afisaa mmoja wa polisi aliyeomba kubanwa jina amesema mwanamke huyo anaendelea kupata nafuu katika hospitali kuu ya wilaya ya Naivasha, huku mwili wa marehemu mumewe ukihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali iyo hiyo.