Mahakama ya Mombasa imemuachilia huru mwanamume mwenye umri wa miaka 20 aliyepigwa na kupata majeraha mabaya ya uso, kwa kudaiwa kuiba nazi.
Mshtakiwa, Mohamed Kibunda, anadaiwa kuiba nazi tano zenye thamani ya shilingi 240, mali ya Abdulkadir Mwinyi, huko Kibundani mnamo Februari 23, mwaka huu.
Mshtakiwa huyo alikubali shtaka hilo la kutekeleza wizi huo wa nazi mbele ya Hakimu Diana Mochache.
Akitoa uamuzi wake siku ya Jumatano, Hakimu Mochache alisema kuwa kichapo alichopewa jamaa huyo ni funzo tosha, hivyo basi kuamuachilia huru ili apate matibabu ya haraka.