Mwakilishi wa Wadi ya Kadzandani, Mohamed Ndanda, ametangaza wazi azimio lake la kuwania kiti cha ubunge katika eneo bunge la Nyali.
Ndanda aliyasema haya siku ya Jumapili katika eneo la Kongowea, muda mchache tu baada ya mbunge wa Nyali Hezron Awiti kutangaza kuwania kiti cha ugavana katika Kaunti ya Mombasa.
Ndanda aliahidi kumuunga mkono Awiti katika kuwania kiti hicho cha ugavana, akisema kuwa malengo yao ni kubadilisha uongozi wa Kaunti ya Mombasa.
Ndanda aliongeza kuwa haridhishwi na uongozi wa sasa wa serikali ya Mombasa na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpigia kura gavana mtarajiwa Awiti, naye wamchague kama mbunge wa Nyali.
Ndanda alisisitiza kushughulikia kwa haraka matatizo yanayowakumba wakaazi wa Mombasa kama vile ukosefu wa usalama na mizozo ya kibiashara baina ya serikali ya kaunti na wafanyibiashara hao.