Mwanamume mmoja aliyekamatwa mapema hii leo hapa Mombasa akihusishwa na tuhuma za ugaidi amefunguliwa mashtaka mahakamani Mombasa.
Polisi walisema Icrima Mohammed Soshi ni nduguye mshukiwa wa ugaidi Mohammed Soshi anayesakwa na polisi kwa tuhuma sawia na hizo.
Icrima, aliyekamatwa katika mkahawa mmoja wa burudani Mombasa anahusishwa na mauaji ya afisa wa kijasusi katika mtaa wa Old Town mwaka jana.
Inasemekana mshukiwa huyo amekuwa akiwasiliana mara kwa mara na nduguye ambaye ni mmoja wa washukiwa wa ugaidi waliotoroka eneo la majengo mapema wiki hii.
Naibu mkuu wa polisi hapa Mombasa Patrick Njoroge amesema simu yake ya rununu inachunguzwa kwa taarifa muhimu ili kusaidia kwenye kesi dhidi yake.