Mbunge wa Bahati Kimani Ngunjiri ameapa kuimarisha hali ya shule katika eneo bunge lake.
Akizungumza Jumanne wakati wa kutoa hundi ya shilingi elfu 120 za ujenzi wa vyoo katika shule ya sekondari ya Heshima, Ngunjiri alisema elimu ni muhimu kwa jamii, na inahitajika kila mwanafunzi kupata.
"Afisi yangu imejitolea kuhakikisha kwamba shule zote zinaimarishwa katika eneo bunge la bahati," alilsema Ngunjiri.
Wakati huo huo, Ngunjiri alitoa wito kwa serikali ya kaunti ya Nakuru kuhakikisha kwamba ina shule za chekechea zinaimarishwa.
"Shule za chekechea ziko chini ya serikali za kaunti na zinafaa kupigwa jeki ili kuhakikisha watoto wanapata elimu bora," Ngunjiri aliongeza.