Huenda kinyanganyiro cha ugavana katika kaunti ya Nyamira kikaibua joto la kisiasa baina ya aliyekuwa mbunge wa eneo bunge la Kitutu Masaba Walter Nyambati na gavana wa sasa wa kaunti hiyo John Nyagarama.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hii ni baada ya wawaniaji wawili wa ugavana Evans Misati, Kinara Ndubi kujitoa rasmi kwenye kinyang'anyiro hicho na kumuunga mkono mwenyekiti wa shirika la uchapishaji vitabu la Jomo Kenyatta siku ya Jumapili. 

Akihutubia wakazi wa Bogwendo mapema Jumapili, Kinara Ndubi alisema kuwa ameamua kumuunga mkono Nyambati kwa maana ana hakika kuwa huenda Nyambati akampa changamoto gavana Nyagarama kutokana na sababu kwamba ana ushawishi mkubwa kwenye maeneo ya uwakilishi bunge kote Nyamira. 

"Sitaki kuwa kwenye kinyanganyiro cha uwaniaji ugavana ikiwa kwamba mwenyekiti wa shirika la Jomo Kenyatta Foundation amejitosa na nina hakika kwamba ana ushawishi mkubwa kote Nyamira na hata pia rekodi yake ya maendeleo ni ya kutiliwa mfano," alisema Ndubi. 

Kwa upande wake, Evans Misati alisema kuwa kwa minajili ya shughuli za kikazi ambazo ndiyo sababu yake ya kumuunga mkono Nyambati ikizingatiwa kwamba ana uwezo wa kuwaunganisha watu wa Kitutu Masaba.

"Nadhani kwamba Nyambati anaweza akawaunganisha watu wa Kitutu Masaba kwa maana tuna idadi kubwa ya wapiga kura na sababu ya shughuli za kikazi zinazonibana naona ni kheri nimuunge mkono Nyambati," alihoji Misati.