Mbunge wa eneo bunge la Mugirango Kusini Manson Nyamweya ameiomba Serikali ya kaunti kutumia pesa za wananchi vizuri ili kuleta maendeleo zaidi.
Akizungumza siku ya Jumapili mjini Kisii, Nyamweya alisema serikali ya Kaunti ya Kisii hupokea mabillioni ya pesa kama kaunti zingine kila mwaka, na kuna haja ya pesa hizo kutumika vizuri kufanya maendeleo kikamilifu.
“Pesa ambazo serikali ya Kaunti ya Kisii inapokezwa zinastahili kufanya maendeleo sawia kwa maeneo bunge yote tisa yalioko katika kaunti hii,” alisema Nyamweya.
Aliongeza, “Ikiwa serikali inahitaji wananchi kufurahia uongozi uliopo kwa sasa, sharti maendeleo yashuhudiwe kikamilifu.”
Miongoni mwa maendeleo ambayo Nyamweya aliomba serikali kufanya ni kuweka miradi ya maji katika kila wadi ili kuwapa afueni akina mama, na kukarabati barabara kikamilifu, haswa zile ambazo
Nyamweya pia alimtaka Gavana James Ongwae kutimiza ahadi za maendeleo alizowaahidi wakazi wa kaunti hiyo wakati wa kampeini.
“Unapotoa ahadi wakati wa kutafuta kura, unastahili kutimiza ahadi hizo ili kuunda uhusiano mwema na wakazi,” alisema Nyamweya.
Nyamweya alisema kuwa atakutana uwanjani na Ongwae kupimana nguvu katika uchaguzi mkuu ujao.