Share news tips with us here at Hivisasa

Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae ameahidi kuleta wawekezaji wengi kuwekeza katika kaunti hiyo ili kuinua uchumi wa kaunti pamoja na taifa la Kenya kwa ujumla.

Hii ni baada ya baadhi ya kampuni kuitikia kuwekeza katika kaunti hiyo biashara ya shillingi billioni 21.

Akizungumza siku ya Jumapili mjini kisii baada ya kongamano la wafanyibiashara kukamilika siku ya Jumamosi, Ongwae alisema tayari ametia sahihi na kampuni zingine ili kuwekeza katika kaunti hiyo. 

Ongwae alisema maisha ya wakazi wa kaunti hiyo yatabadilika pakubwa chini ya uongozi wake kwani alichaguliwa kufanya maendeleo

Miongoni mwa kampuni ambazo zimetia sahihi kuwekeza katika kaunti ya Kisii ni kampuni ya Kanuria kutoka taifa la India ambayo itaanzisha kiwanda cha sukari na nguvu za umeme kwa billioni 5, kampuni ya Booring kutoka taifa la China ambayo itaanzisha kiwanda cha kutengeneza kokoto kwa billioni 10.

“Mimi kama gavana nitahakikisha kuwa wawekezaji wengi wamekuja na kuwekeza katika kaunti hii ya Kisii maana nahitaji kuona maisha ya wakazi yako salama na kuinua uchumi wa kaunti na taifa letu la Kenya,” alisema Ongwae.