Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae ameahidi kufanya maendeleo mengi zaidi kabla ya uchaguzi ujao wa mwaka wa 2017.

Kulingana naye, alichaguliwa na wapiga kura ili kuwatumikia wakazi wa kaunti hiyo kimaendeleo na kuinua uchumi wa kaunti kwa jumla.

Akizungumza siku ya Jumamosi katika uwanja wa Gusii Stadium wakati wa kusherekea siku ya Jamuhuri, Ongwae alisisitiza kuwa atainua viwango vya uchumi. 

Aidha, Ongwae pia alikariri kuwa katika kaunti ya Kisii kuna masoko 52 ambayo aliweka katika ratiba ili kukarabatiwa kama njia moja ya kuimarisha mazingira ya wafanyibiashara, na kufikia sasa, masoko 32 tayari yamekarabatiwa kikamilifu huku akiahidi kukarabati hayo mengine  kabla ya mwaka wa 2017.

“Mlinichagua kuwa gavana wa Kaunti hii ya Kisii ili niwaletee maendeleo, na yale tayari nimefanya mnaweza yaona sitaki niyaseme lakini nitafanya mengi zaidi kabla ya mwaka wa 2017 kufika,” alisema Ongwae.

Wakati huo huo, gavana huyo alisema kila wadi ya kaunti hiyo itakarabatiwa barabara kilomita tano ili kurahisisha sekta ya uchukuzi kwa wafanyibiashara na wakulima.

Ata hivyo, aliwaomba wawakilishi wadi na mawaziri wa serikali yake kushirikiana naye kuhakikisha maendeleo yamefanywa kwa ujumla.

“Naomba ushirikiano mwema kutoka kwa wawakilishi wadi na mawaziri ili tulete maendeleo kwa kaunti yetu,” aliongeza Ongwae.