Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae ameahidi kuajiri wahudumu wa afya katika hospitali ya Misesi kaunti ya Kisii ili kuboresha huduma za matibabu katika hospitali hiyo.
Ongwae alisema alitaja changamoto zinazokumba hospitali hiyo kuwa upunguvu wa wahudumu wa afya na mashine za kupima magonjwa na kutoa ahadi ya kutafuta suluhu halisi hivi karibuni.
Akizungumza siku ya Jumapili mjini Kisii Ongwae alisema ataongeza wahudumu wa afya katika hosptali hiyo na kununua baadhi ya mashine amabazo zitatumika kupima magonjwa ya kimwili haswa damu na mengine mengi.
“Nilitembelea hospitali ya Misesi level 4 nikaona yale ambayo yamekosa katika hospitali hiyo na nitaongeza wahudumu wa afya na kununua baadhi ya mashene ambazo zinahitajika ili sekta ya afya iwe kamifu katika hospitali hiyo,” alisema Ongwae.
“Serikali yangu hushughulikia kila mradi haswa sekta ya afya kwani kila mtu anahitaji afya na ni lazima mimi kama gavana nihakikishe hospitali zilizoko hapa kwa kaunti ya Kisii zinatoa huduma bora ya matibabu,” aliongeza Ongwae.
Gavana Ongwae ameonekana kupea kipau mbele sekta ya afya katika kaunti yake baada ya wakaazi wa kaunti hiyo kuomba matibabu katika hospitali mbalimbali kuboreshwa, jambo ambalo limeonekana kukubaliwa na gavana wao kwani sekta hiyo ndio ya muhimu kwa maisha ya binadamu.