Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wabunge wote wa Kaunti ya Kisii wakiongozwa na mbunge wa eneo bunge la Nyaribari chache Richard Tong’i wameahidi kufanya kazi na gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae ili kuleta maendeleo zaidi  kwa weananchi wa kaunti hiyo.

Hii ni baada ya Gavana wa kaunti hiyo  James Ongwae mapema wiki hii kuomba wabunge wa kaunti hiyo kuacha na kusahau masuala ya kisiasa na mambo ya uchaguzi wa  mwaka 2013 ili kufanya kazi pamoja na kuinua maendeleo katika kaunti ya Kisii.

Akizungumza siku ya Ijumaa mjini Kisii, Tong’i, mbunge wa Kitutu Chache Kusini Richard Onyonka na wengine waliahidi kushirikana na gavana ili kuleta maendeleo mengi zaidi katika kaunti ya Kisii.

“Gavana wetu hukuingia katika kiti cha ugavana kimakosa. Ulichaguliwa na wananchi, ingawa niko katika upande wa  serikali ya Jubilee nitashirikiana nawe kufanya maendeleo katika kaunti yetu,” alisema Tong’i.

“Hata wabunge wengine wamejitolea kufanya kazi nawe hadi mwaka wa 2017 lakini kwa sasa yale tunahitaji kufanya ni maendeleo si mambo ya kisiasa."

Aidha, mbune Onyonga naye aliunga mkono matamshi ya Bw Tongi kwa kusema atafanya kazi na Gavana Ongwae ili wananchi kufurahia viongozi waliowachagua kuwafanyia maendeleo.

“Gavana, tuko pamoja kwa maendeleo na tumejitolea kushirikiana na wewe,” alisema Onyonka.