Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae amesema serikali yake itaunganisha mitandao ya bure bila malipo mjini Kisii, ambayo ili kutumiwa na wakazi pamoja na wafanyibiashara wa mji huo kuinua uchumi na biashara.

Kulingana na Ongwae, ni vizuri mji wa Kisii kuunganishiwa na mitandao hiyo aina ya ‘WI-FI’ ili kuinua biashara na kusaidia wafanyibiashara na wawekezaji wanapofanya shughuli zao za kibiashara.

Akizungumza siku ya Jumanne afisini mwake wakati alikuwa anatia sahihi makubaliano na kampuni ya E-Telecom ambayo itawekeza WiFI ya bure, Ongwae alisema siku zijazo angependa kuona mji wa Kisii ukiwa na mtandao huo. 

“Mji wa Kisii katika siku zijazo utakuwa na mabadiliko makubwa ili wawekezaji wanapokuja kuwekeza hapa na wafanyibiashara wengine wawe wanafurahia WI-FI ya bure, serikali yangu itaweka mikakati kabambe kuhakikisha yote yamefanywa,” alisema gavana Ongwae.

Aidha gavana huyo aliahidi kuleta maendeleo mengi zaidi katika kaunti hiyo na kusema atahakikisha ahadi zote alizotoa kwa wakazi wakati wa kampeni amezitimiza ili kuonyesha uongozi wa vitendo.

“Serikali yangu itajaribu kila iwezalo kuona yale wakazi wanahitaji kufanyiwa yamefanywa kwa wakati unaofaa,” aliongeza Ongwae.