Share news tips with us here at Hivisasa

Kamishna wa kaunti ya Nyamira Josphine Onunga amewaonya vikali wakazi dhidi yakuchukua sheria mikononi mwao kwa kuwaadhibu washukiwa wa wizi. 

 Akihutubia wakazi mjini Nyamira siku ya jumatano wiki iliyopita, Onunga alisema kuwa visa vya baadhi ya wananchi kuchukua sheria mikononi mwao kwakuwachapa washukiwa wa uhalifu vinaendelea kuongezeka katika maeneo mengi ya kaunti hali iliyomlazimu kuwaonya wananchi dhidi ya mazoea yakuchukua sheria mikononi mwao. 

"Ni jambo lakushangaza kuwa visa vya wananchi kuchukua hatua nakuwapiga washukiwa wa uhalufu vinaendelea kushamiri katika maeneo mengi Nyamira na sharti kila mmoja wetu aheshimu sheria kwa kuwa kuwapiga washukiwa wa wizi kwa nia yakuua ni kinyume cha sheria na kamwe hilo haliwezi kuruhusiwa," alionya Onunga. 

Onunga aidha aliwasihi wananchi kuwasilisha washukiwa hao kwa maafisa wa polisi pindi tu wanapowashika badala yao kuchukua sheria mikononi mwao.  

"Nawahimiza wananchi kuwashika na kisha kuwawasilisha washukiwa wa aina hiyo kwa maafisa wa polisi ili hatua kuchukuliwa dhidi yao badala yakuchukua sheria mikononi mwenu kwakuwachapa washukiwa kwa nia yakuwaua," alisihi Onunga. 

Haya yanajiri baada ya washukiwa wawili wa wizi wakimabavu walipelekwa kupokea matibabu kwenye hospitali kuu ya Kisii baada ya wakazi wa Nyamira mjini kuwapa kichapo cha umbwa mapema wiki jana.