Wahudumu wa Matatu mjini Kisii wamemwomba mbunge wa eneo bunge la Kitutu Chache kusini Richard Onyonka kukarabati barabara ya kutoka mjini Kisii kuelekea eneo la Nyamataro–Nyakoe, barabara ambayo imeonekana kuwa mbovu zaidi.
Hii ni baada ya barabara hiyo ambayo ina mashimo kadhaa, na kuomba msaada kutoka kwa mbunge Onyonka, kwani barabara hiyo inastahili kutengenezwa na serikali ya kitaifa..
Wakiongea na waandishi wa habari mnamo siku ya Alhamisi katika kituo cha magari mjini Kisii, wahudumu hao wakiongozwa na Dereva Jadson Makori walimtaka Onyonka kukarabati barabara hiyo ambayo imekuwa mbovu.
Wakati huo huo, wahudumu hao walisema hii si mara yao ya kwanza kuomba mbunge huyo kukarabati barabara hizo na kusema wataandamana ikiwa hatakarabati barabara hiyo kwa wiki tatu zijazo.
“Barabara ya Kisii-Nyamataro-Nyakoe imechimbuka na ina mashimo mengi tunaomba mbunge Richard Onyonka kuikarabati barabara hiyo kama anahitaji amani,”alisema Makori.
“Tumekuwa tukisema kila wakati, lile tumesalia nalo ni kufanya maandamano kumlazimu mbunge kuitikia wito wetu,” alisema Victor Mogonga dereva mwingine.