Kanisa la PCEA limehimiza wakristo kueneza ujumbe wa IEBC kuhusu usajili wa wapiga kura.
Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa la PCEA Dr Arthur mjini Nakuru, mchungaji James Mwangi Munene alisema kuwa wakristo wana wajibu mkubwa katika shughuli nzima.
Kwa mujibu wake swala hilo halifai kuachiwa tu wanasiasa bali ni wajibu wa kila mmoja.
"Ombi langu tu ni kwamba wakristo tushiriki katika kueneza ujumbe huu ili watu wajisajili kwa wingi kama wapiga kura," Munene alisema.
Wakati huo huo, aliwataka wazazi kuwahimiza wanao kuhusu umuhimu wa zoezi hilo.