Share news tips with us here at Hivisasa

Mawakili wa serikali sasa hawataweza kuhifadhi hela katika benki za kigeni baada ya mwanasheria mkuu Githu Muigai, kuzindua sheria mpya itakayo wazuia kufanya biashara na benki hizo.

Kulingana na sheria hiyo, mawakili hao hawataruhusiwa kua na umiliki katika taasisi za serikali, hatua inayolenga kuzuia mgongano wa maslahi wakati wa kutoa uamuzi katika kesi inayohusu taasisi zinazowahusu au familia zao.

Aidha, mawakili hao watahitaji kibali na idhini ya kutoka tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi nchini EACC iwapo watataka kuhifadhi hela katika benki za kigeni.

Kwa mujibu wa mwanasheria mkuu, sheria hiyo, inalenga kuimarisha maadili miongoni mwa mawakili wa serikali.