Share news tips with us here at Hivisasa

Sekta ya utalii nchini imepata pigo jingine baada ya kampuni ya International SOS kuorodhesha sehemu zinazovutia watalii nchini kuwa miongoni mwa sehemu zisizo salama kwa wageni.

Katika utafiti wake, kampuni hiyo, ambayo hufanya utafiti kuhusu usafiri na maswala ya kiafya ulimwenguni, imetoa ripoti inayosema kuwa mji wa Nairobi na Mombasa si salama kwa wageni wanaozuru nchini.

Kwa mujibu International SOS, Samburu, Pokot magharibi, Marsabit, Isiolo, Garissa magharibi na Lamu ni maeneo ambayo si salama kwa watalii.

Kulingana na ripoti hiyo, hali ya usalama iko chini Kenya ikilinganishwa na mataifa jirani kama Uganda na Tanzania.

Haya yanajiri wiki moja tu baada ya taifa la Ufaransa kuondoa marufuku ya kutozuru Kenya lililoyawekea wananchi wake.

Hata hivyo, ripoti hiyo haitarijiwi kuathiri sekta ya utalii kwani mji wa Mombasa tayari umeshuhudia ongezeko la wageni msimu huu wa Krismasi ikilinganishwa na 2014.