Polisi Kithimani wanawasaka wanaume wawili waliompiga mhudumu wa bodaboda na kumwibia pikipiki yake katika Soko la Kithimani.
Akidhibitisha kisa hicho siku ya Jumatatu, OCPD was Yatta, Edward Kipsang, alielezea kuwa wanaume hao walijifanya kuwa wateja na baadaye kumvamia mhudumu huyo na kumwacha na majeraha kabla ya kuondoka na pikipiki yake.
"Ilikuwa mwendo was saa sita usiku mwanamume huyo alipovamiwa na majambazi waliojifanya kuwa wateja. Majambazi hao walimpiga na kisha kutoroka na pikipiki hio,” alisema Kipsang.
Kipsang alisema kuwa wahudumu wengi wa bodaboda wamekuwa wakipuuza wito kutoka kwa maafisa was polisi wa kufunga kazi baada ya saa tano usiku ili kupunguza visa vya wizi.
Aidha, afisa huyo aliwaomba wenye vibanda vya kuuza miraa kufunga kazi zao mapema kwani inakisiwa majambazi wengi wanaowaibia watu hujificha katika vibanda hivyo.