Share news tips with us here at Hivisasa

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Mombasa wameagizwa kushika doria kila usiku na mchana na kuwa macho zaidi kutokana na hali ya vuta nkuvute baina ya viongozi mbali mbali katika kaunti hiyo.

Mkuu wa polisi katika kanda ya Pwani Francis Wanjohi amesema kuwa kuna kundi la vijana wahalifu ambao watachipuka katika wakati huu kwa maadai ya kuwaunga viongozi wao mkono na kutumia fursa hii kutekeleza uhalifu.

“Kuna baadhi ya watu ambao watajifanya kumuunga mkono kiongozi fulani na kutumia fursa hii kufanya uhalifu,” alisema Wanjohi.

Hata hivyo afisa huyo amewahakikishia wakaazi kuwa maafisa wa polisi watatimiza wajibu wao wa kulinda amani na utulivu katika kaunti zote za Pwani.